Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo
Awesome Image

Utalii wetu wa Zanzibar ni utalii wa bahari. Ni utalii unaotegemea uhai na afya ya bahari na rasilmali zake. Hivyo Utalii Endelevu ni ule unaojali hifadhi za maeneo ya bahari, bioanuwai ya bahari, usafi na mazingira safi ya fukwe na bahari zake. Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi inapigania sana Utalii Endelevu wa Zanzibar unaojali mazingira ya bahari pamoja na mila na desturi za watu wa Zanzibar.
Serikali itahakikisha uhifadhi wa mila, desturi na tamaduni za nchi, chini za kaulimbiu ya “Utalii Endelevu kwa Wote”, unaozingatia ustawi wa jamii, utalii wa ndani wa unaotunza mazingira na usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani.

Vipaumbele vikuu vya Utalii Endelevu kwa Zanzibar ni pamoja na:

• Kukuza matamasha ya kimila na ya kitamaduni na mila za kienyeji katika Uchumi wa Buluu.
• Kuongeza uwelewa kwa watalii juu ya mila na desturi katika maeneo ya ukanda wa pwani.
• Kukuza utalii jumuishi unaozingatia uwekezaji na haki za jamii.
• Kukuza uelewa wa utunzaji wa mazingira na jamii kusimamia rasilimali zao ili kuhakikisha maendeleo endelevu na kuvilinda viumbe vilivyo hatarini kutoweka.
• Kukuza usimamizi shirikishi wa ulinzi na usalama katika maeneo ya kitalii kupitia Mpango Maalumu wa Matumizi ya Bahari.
• Kuimarisha mifumo ya kuifanya Zanzibar iendelee kuwa kivutio kikuu cha utalii; na kutekeleza mpango mkuu wa kuijengea uwezo sekta ya utalii Zanzibar.

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.