Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo

Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar, imeanzishwa rasmi mwezi wa Novemba 2020 na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi, kwa uwezo aliopewa na Kifungu namba 41 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Lengo Kuu la Wizara hii ni kusimamia utekelezaji wa kasi na endelevu wa fursa zilizopo na vipaumbele vyake vya uchumi unaotegemea rasilmali za bahari au Uchumi wa Buluu ili kuijenga Zanzibar mpya yenye uchumi wa kisasa. Wizara inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia matumizi na usimamizi endelevu wa bahari na ukanda wa pwani pamoja na kusimamia, kuratibu na kuimarisha fursa za uwezeshaji na uwekezaji katika sekta za uvuvi, mazao ya baharini, kilimo cha mwani na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 “Vision 2050” imeiweka sekta ya Uchumi wa Buluu kuwa sekta kuu ya kukuza uchumi wa Zanzibar ili kuitoa Zanzibar katika umasikini na kuifikisha kuwa nchi yenye kipato cha kati cha hali ya juu (Upper Middle Income). Mpango wa uimarishaji wa sekta ya Uchumi wa Buluu unaenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025, Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar (ZADEP) wa Mwaka 2021 – 2026, Sera na Mikakati ya Uchumi wa Buluu, Sera ya Uvuvi na Mazao ya Baharini, Sera ya Mafuta na Gesi, pamoja na mipango jumuishi na shirikishi ya sera nyengine mbali mbali za kitaifa zinazohusiana na usimamizi wa bahari na Uchumi wa Buluu.

Halikadhalika, katika utekelezaji wa maazimio na mikataba ya kimataifa, Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ina jukumu la kuhakikisha utekelezaji na ukondoishaji wa mikataba mbali mbali ya kimataifa yanyohusiana na usimamizi wa bahari na Uchumi wa Buluu hususan kwa Zanzibar. Lengo Namba 14 la ‘Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG 14) la Umoja a Mataifa linalohusiana na Usimamizi na Maendeleo Endelevu ya Bahari, Lengo Nambari 6 la Agenda ya Umoja wa Afrika ya Mwaka 2063 (Agenda 2063), pamoja na mikataba na itifaki mbali mbali za kikanda na kimataifa na kikanda inayoongoza na kuhimiza uimarishaji wa Uchumi wa Buluu.

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.