Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo

Idara ya Uendeshaji na Utumishi inahusika na utoaji wa huduma pamoja na kusimamia maslahi ya rasilimali watu ya Wizara, ikiwa ni pamoja na kutunza, kuhuisha na kuhifadhi kumbukumbu za Ofisi. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Majukumu ya Idara ya Uendeshaji na Utumishi ni pamoja na:
• Kutoa huduma za uongozi wa Rasilimali watu na Utawala.
• Kusimamia masuala ya ajira, mafunzo, sifa za utendaji na kupandishwa vyeo.
• Kuweka kumbukumbu za wafanyakazi na kufanya tathmini ya kila muda ya utendaji.
• Kuhifadhi na kutunza kumbukumbu na rasilmali zote za Ofisi.
• Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa mteja.
• Kushughulikia na kukadiria upatikanaji wa mahitaji, vifaa na vitendea kazi.
• Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mkataba wa utoaji wa huduma kwa umma.
• Kusimamia nidhamu na maadili ya watumishi
• Kutafsiri na kusimamia sheria, kanuni na miongozo ya kazi.
• Kuratibu utekelezaji wa upimaji wa utendaji kazi.

Idara ya Uendeshaji na Utumishi inaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni:-
1. Divisheni ya Uendeshaji.
Divisheni hii inahusika na masuala ya utawala, uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kila siku za Ofisi.

2. Divisheni ya Utumishi
Divisheni hii inahusika na masuala ya maendeleo na usimamizi wa rasilimali watu ndani ya Ofisi ikiwemo ajira, mishahara, mafunzo kwa watumishi, upimaji utendaji kazi pamoja na upandishaji vyeo.

3. Divisheni ya Utunzaji wa Kumbukumbu.
Divisheni hii itahusika na shughuli za uwekaji wa kumbukumbu na uhifadhi wa nyaraka na kazi mbali mbali za Ofisi

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.