Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo

Idara hii inahusika na jukumu la kuratibu utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa Buluu ikijumuisha sekta zilizomo chini ya Wizara lakni pia kushirikiana na Sekta za Uchumi wa Buluu zilizo nje ya Wizara. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Majukumu ya Idara ya Maendeleo na Uratibu wa Uchumi wa Buluu ni pamoja na:
• Kusimamia uratibu wa utekelezaji wa Sera na Mkakati wa Uchumi wa Buluu.
• Ufuatiliaji, ushiriki na utekelezaji wa michakato ya kitaifa, kikanda na kimataifa ya Uchumi wa Buluu na Usimamizi wa Bahari wa ujumla
• Kusimamia uendeshaji wa mifumo ya taarifa, mawasiliano na ukuzaji wa ajenda ya Uchumi wa Buluu.
• Kukuza mahusiano na wahisani na wadau wa maendeleo katika maendeleo ya uchumi wa buluu Zanzibar.
• Kuimarisha mashirikiano na Taasisi za Umma, taasisi binafsi na wadau wa maendeleo katika kuendeleza wa Sekta ya Uchumi Buluu.
• Kuibua/ kutafuta fursa na mbalimbali za kuimarisha na kuendeleza sekta ya uchumi buluu Zanzibar.
• Kujenga uelewa kwa taasisi za umma, taasisi binafsi pamoja na wananchi kuhusu maendeleo ya sekta za uchumi wa buluu Zanzibar.

Idara ya Uratibu wa Maendeleo ya Uchumi wa Buluu itaundwa na Divisheni tano (5) ambazo ni:-
1. Divisheni ya Uratibu wa Masuala ya Uvuvi.
Divisheni hii inahusika na kuratibu masuala mtambuka ya Sekta ya Uvuvi.

2. Divisheni ya Uratibu wa Masuala ya Mafuta na Gesi na Nishati Mbadala.
Divisheni hii inahusika na shughuli za uratibu wa masuala ya sekta ya mafuta na Gesi Asilia.

3. Divisheni ya Uratibu wa Utalii Endelevu.
Divisheni hii inahusika na uratibu wa Sekta ya Utalii Endelevu.

4. Divisheni ya Uratibu wa Huduma za Utawala wa Uchumi wa Buluu.
Divisheni hii inahusika na shughuli za kuratibu masuala ya usimamizi wa bahari na sekta za uchumi buluu.

5. Divisheni ya Uratibu wa Biashara na Miundombinu ya Baharini.
Divisheni hii inahusika na kuratibu maendeleo ya miundombinu ya biashara na usafirishaji Baharini.

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.