Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo
Awesome Image

Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ina mpango jumuishi unaohusisha uratibu wa sekta mbali mbali za Uchumi wa Buluu.

Kwa mfano:-

• Kuimarisha ushirikiano wa ulinzi katika ngazi zote ili kuhakikisha kuwepo kwa usalama wa bahari.
• Kuimarisha utayari wa kukabiliana na maafa kwa kuchukua hatua thabiti na za haraka.
• Kuhamasisha kukuza uelewa, kujenga uwezo wa kiufundi na utaalamu juu ya mpango mkuu wa          matumizi ya bahari.
• Kuandaa mbinu bunifu za upatikanaji wa fedha ili kusaidia kukuza Uchumi wa Buluu katika ngazi zote.
• Kuimarisha uwezo wa kufanya tafiti na maendeleo ili kuendana na mahitaji ya maendeleo ya siku              zijazo.
• Kuanzisha mfumo wa usimamizi wa taarifa na takwimu za Uchumi wa Buluu unaozingatia maarifa na    taasisi za utafiti na habari za Zanzibar na kutumia fursa za  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano       (TEHAMA).
• Kuimarisha ushirikiano na mataifa mbalimbali kwa ajili ya kukuza Uchumi wa Buluu na Usimamizi wa        Bahari.
• Kuweka hatua madhubuti za kuzuia VVU/UKIMWI na miripuko katika sekta za Uchumi wa Buluu.
• Kuimarisha uwezo kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum katika Uchumi wa Buluu.
• Kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum katika mipango ya Uchumi    wa Buluu.
• Kukuza ubunifu katika sekta za Uchumi wa Buluu kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum.
• Kuboresha upatikanaji wa soko kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum katika Uchumi wa   Buluu.

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.