Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo
Awesome Image

Mifumo ya Nishati Mbadala ya baharini inakabiliwa na changamoto ya tafiti na maendeleo, hasa katika vyanzo vya nishati mbadala ya upepo, jua na mawimbi. Uwekezaji wa nishati ya jua na upepo baharini bado haujapata ukondoishwaji wa kitaifa wa hali ya juu hapa Zanzibar. Bila ya kuwepo uwezo wa kutosha wa kiufundi, elimu na mtaji wa kifedha maendeleo ya nishati mbadala yatakuwa ni madogo.

Hivyo basi, Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi imejiwekea vipaumbele vifuatavyo:

• Kukuza tafiti na maendeleo katika mifumo ya nishati mbadala kitaifa na kikanda.
• Kuimarisha uwekezaji wa ushirikiano wa pamoja kati ya serikali na sekta binafsi katika mifumo ya nishati mbadala baharini.
• Kuongeza uwezo wa wataalam wa ndani katika kushughulikia nishati mbadala kwa kuwapatia taaluma na uelewa, mafunzo na elimu, na upembuzi yakinifu za kimkakati.
• Kuimarisha tafiti za nishati mbadala za baharini kwa kuweka mifumo endelevu ya kifedha.
• Kuendesha mifumo ya kifedha kwa ajili ya uwekezaji wa nishati mbadala endelevu na yenye kusimamiwa vizuri.
• Kusimamia utekelezaji wa sheria za uhifadhi wa misitu ya mwambao na maeneo muhimu ya makaazi ya viumbe maji.
• Kukuza uelewa wa jamii juu ya faida za nishati mbadala kupitia uhifadhi wa pwani maeneo ya pwani.
• Kuanzisha kitengo maalumu cha nishati mbadala baharini kitakachoshirikisha wadau wa sekta mbalimbali.

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.